www.fgks.org   »   [go: up one dir, main page]

Pata taarifa kuu

Manchester City kucheza dhidi ya Chelsea katika mechi ya kwanza ligi kuu ya EPL

Klabu ya Manchester city itacheza mechi yake ya kwanza ya msimu mpya ugenini dhidi ya Chelsea kwa mujibu wa ratiba mpya ya Ligi kuu ya Uingereza.

Manchester City walishinda ligi msimu uliopita.
Manchester City walishinda ligi msimu uliopita. AP - Dave Thompson
Matangazo ya kibiashara

Manchester city watakuwa na kibarua cha kutetea taji la Premier League msimu huu baada ya kuinyakua msimu uliopita.

Katika mechi yake ya kwanza tarehe 18 ya mwezi Agosti msimu huu Pep Guardiola, atacheza dhidi ya aliyekuwa msaidizi wake awali Enzo Maresca, ambaye aliteuliwa kuwa mkufunzi mkuu wa klabu ya Chelsea mapema mwezi huu.

Maresca, aliteuliwa kuwa kocha wa Chelsea baada ya kuiongoza timu ya Leicester na kufuzu daraja msimi uliopita.

Pep Guardiola- Kocha wa Manchester City
Pep Guardiola- Kocha wa Manchester City AP - Dave Thompson

Kwingineko mabingwa wa kombe la FA Manchester united watakuwa wenyenji katika mechi ya ufunguzi msimu huu dhidi ya Fulham mnamo Agosti 16 ugani Old Trafford.

Mnamo Agosti 17, Ipswich, ambao wamefuzu kushiriki ligi kuu ya Uingereza tena baada ya kushushwa daraja sasa watamkaribisha kocha mpya wa Liverpool Arne Slot anayechukua nafasi yake kocha wa miaka mingi katika timu hiyo Jurgen Klopp.

Leicester, ambao wamerejea katika Ligi Kuu, watacheza dhidi ya Tottenham mnamo Agosti 19.

Wachezaji wa Arsenal wakati wa mechi ya msimu uliopita katika ligi kuu ya Uingereza.
Wachezaji wa Arsenal wakati wa mechi ya msimu uliopita katika ligi kuu ya Uingereza. AFP - PAUL ELLIS

Fabian Hurzeler akiwa Brighton ataanza kazi yake ugenini dhidi ya Everton huku kocha mpya wa West Ham, Julen Lopetegui, akikaribisha Aston Villa.

Arsenal yake Mikel Arteta, ambayo ilimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya City kwa misimu wa pili mfululizo, itawaalika Wolves.

Na Felix Musyoki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.