www.fgks.org   »   [go: up one dir, main page]

Pata taarifa kuu

Kenya, DRC kabaruani, Cameroon yafanya kweli mechi za kufuzu kombe la dunia la FIFA

Mechi za kufuzu kucheza fainali ya kombe la dunia kwa nchi za Afrika zimeendelea kupigwa, timu zikichuana katika viwanja mbalimbali kusaka tiketi hiyo.

Picha kutoka maktaba: Wachezaji wa timu ya taifa ya Cameroon wakishangilia wakati wa mechi za fainali za kombe la mataifa ya Afrika zilizofanyika Ivory Coast. Januari 23, 2024.
Picha kutoka maktaba: Wachezaji wa timu ya taifa ya Cameroon wakishangilia wakati wa mechi za fainali za kombe la mataifa ya Afrika zilizofanyika Ivory Coast. Januari 23, 2024. AFP - KENZO TRIBOUILLARD
Matangazo ya kibiashara

Cameroon, ambao walikuwa wenyeji wa Cabo Verde walijivunia ushindi wa mabao 4-1, ushindi huu ukiifanya Cameroon kuongoza kundi D kwa alama 7, mbele ya Libya kwa tofauti ya bao moja.

 

Cameroon pamoja na Libya zimecheza jumla ya mechi tatu ambapo zote zimeshinda mechi mbili na kupata sare moja.

 

Kwingineko katika kundi A Misiri iliendelea kulinda nafasi yao ya Kwanza, kwa alama 9 wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja.

 

Alhamisi wiki hii, misiri walikuwa wenyenji wa Burkina Faso, ambapo walipata ushindi wa 2-1.

 

Djibout walipoteza mechi dhidi ya wenyeji Sierra Leon jumatano na kufanaya timu hiyo kusalia nafasi ya 6 katika kundi A.

 

 Djibout watakuwa wenyenji katika mechi yao ya nne ambapo watachuana na Ethiopia.

 

Adhaa, Gambia ilipata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Seychelles siku ya Jumamosi na kuiweka timu hiyo katika nafasi ya 5 huku Seychelles ikisalia nafasi ya 6 baada ya kupoteza mechi zote.

 

 Mechi zinazotarajiwa kuchezwa Jumapili 09 /06 /2024.

kundi A: Djibout VS Ethiopia

 

kundi B: Congo DR vs Togo

              Mauritania vs Senegal

 

kundi H: Sào Tomè vs Liberia

             Namibia vs Tunusia

 

Na Felix kyalo Musyoki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.