www.fgks.org   »   [go: up one dir, main page]

Pata taarifa kuu

Novak Djokovic kushiriki michezo ya Olimpiki jijini Paris: Kamati ya Olimpiki

Bingwa wa zamani wa tenesi Duniani Novak Djokovic, atashiriki michezo ya Olimpiki msimu wa Majira ya Joto jijini Paris, kwa mujibu wa Kamati ya Olimpiki ya Serbia.

Hata hivyo, kwa upande wake Djokovic bado hajathibitisha ikiwa atashiriki au la.
Hata hivyo, kwa upande wake Djokovic bado hajathibitisha ikiwa atashiriki au la. © Pierre René-Worms/RFI
Matangazo ya kibiashara

"Novak Djokovic na Dusan Lajovic wamekidhi masharti kulingana na viwango vya ATP na wamethibitishwa kushiriki katika michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Paris 2024," kamati ya Serbia ilisema kwenye tovuti yao Jumanne.

Hata hivyo, kwa upande wake Djokovic bado hajathibitisha ikiwa atashiriki au la.

Mapema mwezi Juni, mshindi huyo wa mara 24 wa Grand Slam alijiondoa kabla ya robo fainali yake ya Roland Garros dhidi ya Casper Ruud baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa alikuwa na jeraha kwenye goti lake.

Bingwa wa zamani wa tenesi Duniani Novak Djokovic, atashiriki michezo ya Olimpiki msimu wa Majira ya Joto jijini Paris, kwa mujibu wa Kamati ya Olimpiki ya Serbia.
Bingwa wa zamani wa tenesi Duniani Novak Djokovic, atashiriki michezo ya Olimpiki msimu wa Majira ya Joto jijini Paris, kwa mujibu wa Kamati ya Olimpiki ya Serbia. © Pierre Rene-Worms RFI

Djokovic, amethibitisha kuwa amefanyiwa upasuaji na hali yake imeimarika japo hajatamka siku ya kurejea uwanjani.

Djokovic amesema kwa muda mrefu kuwa ataipa kipaumbele michezo ya Olimpiki msimu huu wa joto anapofukuzia medali ya dhahabu kwa mchezaji mmoja mmoja.

"Olimpiki ya Paris ni muhimu sana. Olimpiki imekuwa kipaumbele kwangu daima," Djokovic alisema kabla ya msimu wa mashindano ya tenisi, Monte Carlo.

Djokovic, ameshiriki katika mashindano ya olimpiki mara nne na kushinda medali ya shaba mwaka wa 2008 huko Beijing. Djokovic, alipoteza mashindano ya medali na shaba kwa Juan Martin del Potro huko London mwaka 2012. Vilevile alipoteza tena kwa raia margentina, miaka minne baadaye katika raundi ya kwanza huko Rio.

Na Felix Kyalo

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.