Wimbo wa kibaguzi watia doa ushindi wa Argentina wa Copa America

cx

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Argentina walikuwa wakisherehekea ushindi wao katika fainali ya Copa America dhidi ya Colombia
  • Author, Tim Vickery
  • Nafasi, BBC

Argentina imeshinda Copa America, lakini imepoteza heshima ya wengi kwa namna ya usherehekeaji wao.

Kiungo wa timu hiyo Enzo Fernandez anakabiliwa na kesi ya kinidhamu huko Chelsea, baada ya kuchapisha video kwenye mtandao wa kijamii ambayo Shirikisho la Soka la Ufaransa linasema ina "lugha ya ubaguzi na ubaguzi wa rangi.”

Fifa pia inachunguza video hiyo, ambapo wachezaji kadhaa wa kikosi cha Argentina - wakisherehekea ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Colombia katika fainali - wanaimba wimbo ulioimbwa awali na mashabiki wa Argentina, wanaohoji asili ya wachezaji weusi na wachezaji wenye asili ya mchanganyiko wa timu ya Ufaransa.

Pia unaweza kusoma

Argentina kwenyewe

Naibu katibu wa michezo, alipendekeza nahodha wa timu Lionel Messi na rais wa FA wa nchi hiyo Claudio Tapia, waombe radhi kwa wimbo huo ambao baadhi ya wachezaji walikuwa wakiimba kwenye basi siku ya Jumapili usiku.

Garro alifukuzwa kazi siku ya Jumatano kwa maoni hayo, huku wengine wakikataa hitaji la kuomba msamaha.

Katika baadhi ya matukio ya kuchukiza na kuhuzunisha, wakati timu kutoka Argentina zinapocheza na wapinzani kutoka Brazili katika mashindano ya vilabu vya bara, kuna matukio ya mashabiki wa Argentina kufanya ishara za nyani.

Walipohojiwa, wahusika walikanusha vikali kwamba wao si wabaguzi. Chochote kinachomuudhi mpinzani ni sawa. Na hisia kama hizo zimeenea Argentina.

Majaribio ya vilabu vya Argentina kukabiliana na tabia hii mara nyingi yamekwama, huita ni 'chuki dhidi ya wageni' - badala ya kuiita ni ubaguzi wa rangi.

Kinachosikitisha zaidi ni ukweli kwamba tabia hii imeonyeshwa na baadhi ya wachezaji. Hapa hakuna kisingizio.

Ukiondoa golikipa mmoja wa akiba, kikosi kizima cha Argentina kinacheza Ulaya.

Asili ya wimbo huo

xz

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Enzo Fernandez aliomba msamaha baada ya kutuma video kwenye mtandao wa kijamii ambayo Shirikisho la Soka la Ufaransa lilisema ni wa "kibaguzi."

Maneno ya wimbo huu, ambao uliibuka katika fainali ya Kombe la Dunia Qatar, ambapo Argentina ilishinda kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Ufaransa, yanaudhi sana.

Wachezaji wa Argentina wanahatarisha sio tu kuwatusi wachezaji wenzao weusi na mashabiki. Nyimbo hizi zinatukana pia urithi wao wenyewe.

Ni nadra siku hizi kuona Muargentina mweusi. Lakini historia haiku hivyo.

Tukirejea enzi za utawala wa kikoloni wa Uhispania, nchi hiyo iliingiza Waafrika wachache sana waliokuwa watumwa kuliko nchi jirani ya Brazili, na ilikomesha utumwa mapema zaidi.

Lakini karibu miaka mia mbili iliyopita, mji mkuu wa Buenos Aires ulikuwa na watu wengi weusi.

Matokeo ya Ubaguzi wa rangi

dfc

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mashabiki wa Argentina wakishangilia katika mitaa ya Buenos Aires baada ya kuifunga Colombia katika fainali ya Copa America

Kuna nadharia nyingi, moja ni milipuko ya homa ya manjano na vifo katika vita vya kupigania uhuru, ndiyo yaliyofanya watu weusi kupotea.

Lililo la kweli hasa, watu hao walimezwa na mamilioni ya wahamiaji waliomiminika kutoka Ulaya na Mashariki ya Kati (hasa Italia - Waajentina wanazungumza Kihispania kwa lafudhi ya Kiitaliano) mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20.

Watu wenye ngozi nyeusi mara nyingi hupewa jina la utani 'el negro' - ambalo halina maana mbaya. Historia ya Waafrika imeacha alama yake. Muziki muhimu zaidi katika utamaduni wa Argentina ni tango. Neno hilo ni la Kiafrika.

Na muziki wa dansi, kama aina nyingi za miziki ya Amerika, ni matokeo ya mchanganyiko wa mitindo ya Kiafrika, Ulaya na jamii za asili.

Kwa sababu ya asili yake tango, muziki huo ulidharauliwa na watu wa hadhi ya juu wa Argentina - hadi ulipokuwa maarufu huko Paris mwanzoni mwa karne ya 20 na hivyo kupendwa Argentina.

Kama vile muziki wa samba huko Brazil, tango huko Argentina. Ni aina ya muziki ambayo ilianza chini katika jamii na kuhamia juu.

Rafiki yangu ambaye ni mwanasosholojia mweusi kutoka Uruguay, ameishi kwa miaka mingi huko Buenos Aires bila kukumbana na shida hata kidogo.

Kwa upande mwingine, kuwepo tu kwa wahamiaji wengi kutoka Ulaya katika eneo la kusini ya Amerika Kusini ulikuwa ni mradi wa ubaguzi wa rangi.

Wakati huo, kulikuwa na mawazo na imani kwamba baadhi ya jamii ni bora kuliko nyingine.

Viongozi wa Amerika Kusini walitaka 'kuboresha' na 'kustaarabu' nchi zao kwa kuingiza nguvu kazi Wazungu.

Kuwepo kwa watu wengi Wazungu wenye asili ya Ulaya huko Argentina ni matokeo ya mawazo ya ubaguzi wa rangi.

Wazo la jamii moja ni bora kuliko nyingine, halijatoweka moja kwa moja, na limeibuka katika mashairi ya wimbo huo ambao baadhi ya wachezaji wa Argentina walitia doa ubingwa wao siku ya Jumapili.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Yusuf Jumah