Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Papa Hormisdas alikuwa Papa kuanzia tarehe 20 Julai 514 hadi kifo chake tarehe 6 Agosti 523[1].
Alimfuata Papa Simako akafuatwa na Papa Yohane I.
Alipochaguliwa alikuwa shemasi mjane; kutokana na ndoa yake alikuwa na mwana aliyekuja kuwa Papa Silverio baadaye.
Mjumbe wa amani katika Kanisa la Magharibi na Kanisa la Mashariki vilevile, alipatanisha waliokuwa wafuasi wa antipapa Laurentius[2] akafaulu pia kumaliza farakano lililoanzishwa na Patriarki Acacius wa Konstantinopoli (484-519)[3] na kufanya waliovamia Ulaya Magharibi waheshimu haki za Kanisa [4].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Agosti[5].
Lua error in package.lua at line 80: module 'Module:Navbar/configuration' not found.
|
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Hormisdas kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|