www.fgks.org   »   [go: up one dir, main page]

Pata taarifa kuu

Comoro yazindua kampeni ya chanjo baada ya vifo 134 vya kipindupindu

Katika visiwa vya Comoro, vilivyoathiriwa kwa miezi minne na mlipuko wa kipindupindu ambao tayari umeua watu 134, kampeni ya chanjo ilizinduliwa Alhamisi huko Anjouan, kisiwa kilichoathiriwa zaidi, kulingana na shirika la habari la AFP likunukuu mamlaka ya afya.

Anjouan ndicho kisiwa chenye watu wengi zaidi katika visiwa vya Bahari ya Hindi, chenye wakazi 330,000 kati ya 870,000 wa nchi hiyo. Kati ya vifo 134 vilivyorekodiwa, Anjouan ina 116, kulingana na taarifa rasmi ya hivi punde ya afya.
Anjouan ndicho kisiwa chenye watu wengi zaidi katika visiwa vya Bahari ya Hindi, chenye wakazi 330,000 kati ya 870,000 wa nchi hiyo. Kati ya vifo 134 vilivyorekodiwa, Anjouan ina 116, kulingana na taarifa rasmi ya hivi punde ya afya. CC BY-SA 3.0/Haryamouji/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya watoto 1,300 wamepokea dozi ya chanjo ya kumeza kwenye kisiwa hiki maskini zaidi cha Comoro kilicho karibu na idara ya Ufaransa ya Mayotte, ambako ugonjwa wa kipindupindu umeua watu wawili tangu mwezi Machi.

"Chanjo itatoa kinga ya miezi sita na hivyo kuvunja mlolongo wa maambukizi," Anssoufouddine Mohamed, mkurugenzi wa afya wa kikanda katika kisiwa hicho, ameliambia shirika la habari la AFP.

Anjouan ndicho kisiwa chenye watu wengi zaidi katika visiwa vya Bahari ya Hindi, chenye wakazi 330,000 kati ya 870,000 wa nchi hiyo. Kati ya vifo 134 vilivyorekodiwa, Anjouan ina 116, kulingana na taarifa rasmi ya hivi punde ya afya.

Muungano wa Visiwa vya Comoro hadi sasa umerekodi visa 8,734 vya ugonjwa wa kipindupindu, baada ya kuzuka kwa ugonjwa huo mapema mwezi wa Februari ulioletwa na meli kutoka Tanzania, ambako ugonjwa wa kipindupindu umeenea.

"Tulianza kwa kuwachanja wanafunzi shuleni kwa sababu hivi karibuni wataenda likizo," ameeleza Bw. Mohamed, daktari wa magonjwa ya moyo. Zaidi ya dozi 270,000 zinapatikana katika kisiwa hicho, lakini "tunahitaji 379,000," alisema Hayiriat Bint Hakim, anayehusika na chanjo, aliyehojiwa na AFP. Kampeni ya majaribio inatarajiwa kudumu kwa siku tano.

"Chanjo hii ni mojawapo ya hatua za kuondoa janga hili inaweza kurejea ikiwa hatua za kuzuia hazitaheshimiwa, kama vile kunawa mikono na kuwa na maji ya kunywa," anaonya mkurugenzi wa afya wa eneo hilo.

Chini ya 30% ya watu wanapata maji ya kunywa, kulingana na maafisa wa kampuni inayohusika na usambazaji wa maji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.