Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wanawikipedia waliojiandikisha wanakaribishwa kwenda ukurasa wa Jumuiya na kupiga kura kuhusu mwonekano wa kurasa zetu
Kamusi Elezo ya Kiswahili
|
Karibu kwenye Wikipedia ya Kiswahili!
Wikipedia ni mradi wa kuandika kamusi elezo kamili na sahihi ya maandishi huru.
Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Tunakushauri ujiandikishe na kufungua akaunti. Angalia Wikipedia:Mwongozo ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia, ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.
|
Je, wajua...
|
|
|
|
|
Picha nzuri ya wiki
|
Duma ni mnyama mbuai aliyemo katika jamii ya paka (Felinae). Chakula chake ni wanyama jamii ya swala hupatikana Afrika na kidogo sehemu za Asia.
Kichwa chake ni kidogo zaidi ukilinganisha na wanyama wengine wa jamii yake kama chui. Duma anatofautiana na chui pia kwa sehemu ya mgongo na sehemu ya machoni: mgongo wa duma huwa kama alama ya "S", tofauti na mgongo wa chui. Macho ya duma yana weusi mkali ukilinganisha na chui.
Ngozi yake ina rangi ya manjano inayoelekea kwenye rangi ya udongo iliyopambwa na madoa meusi. Rangi ya duma inashabihiana na mazingira yake ya mawindo hutegemea zaidi mbio na kuona ukilinganisha na wanyama wengine wawindaji ambao hutegemea kunusa na kuvizia katika mawindo yao. Ndiye mnyama anayeaminika kuwa na mwendo kasi zaidi kuliko wanyama wengine watembeao kwa miguu: hukimbia kilometa 113 kwa saa.
|
|
Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili
- Idadi ya makala: 75,327
- Idadi ya kurasa zote: 154,565 (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
- Idadi ya hariri: 1,253,217
- Idadi ya watumiaji waliojiandikisha: 56,603
- Idadi ya wakabidhi: 14
- Idadi ya watumiaji hai: 97 (Watumiaji waliojiandikisha na kuchangia katika muda wa siku 30 zilizopita)
- Bofya hapa kwa kupata namba za sasa
- Katika mwezi wa Agosti 2020 wikipedia ya Kiswahili iliangaliwa mara milioni 1.73 hivi, ambayo ni sawa na mara 55,800 kwa siku au mara 2,326 kila saa. Asilimia 52 za wasomaji wetu wako Tanzania, asilimia 13 wako Kenya, asilimia 18 wako Marekani na mnamo asilimia 10 wako Ulaya.
- Angalia idadi ya wasomaji kwa makala mbalimbali
- (fungua anwani kwa browser yako, ondoa majina yaliyopo na ingiza jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015 hapa)
- na makala 100 zilizotazamiwa zaidi "Topviews" kwa kipindi fulani.
- (unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku)
Michango ya wanawiki: angalia hapa michango ya mtumiaji kwenye kila mradi wa Wikimedia (andika jina la mtumiaji kwenye sanduku)
Jumuia za Wikimedia
Kamusi elezo ya Wiki ni kamusi elezo huru iliyo chini ya
Shirika Lisilo la Kiserikali la
Wikimedia Foundation, ambalo linasimamia miradi mingine mbalimbali ambayo imeorodheshwa hapo chini. Mpaka sasa miradi inayopatikana Kiswahili ni Wikipedia na Wikamusi. Wikitabu imewekwa Kiswahili lakini bado ni tupu. Mengine inapatikana Kiingereza pamoja na lugha tofauti.
Wikipedia kwa lugha nyingine
Wikipedia kwa lugha nyingine
|
|