Abraham Lincoln

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Picha yake ya kuchorwa.
Uuaji wa Lincoln.

Abraham Lincoln (12 Februari 180915 Aprili 1865) alikuwa Rais wa 16 wa Marekani kuanzia mwaka wa 1861 hadi 1865.

Alikuwa na Kaimu Rais wawili: kwanza Hannibal Hamlin, halafu Andrew Johnson aliyemfuata kama Rais, Lincoln alipouawa.

Lincoln amejulikana kama rais wa upande wa kaskazini katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani kati ya majimbo ya kaskazini dhidi ya shirikisho la kusini.

Kwa hiyo hukumbukwa kama rais aliyeleta mwisho wa utumwa, yaani uhuru kwa watumwa wote wa Marekani na kuunganisha taifa tena.